Aina Ya Website/Blogu Inayoweza Kukuingizia Kipato Ukiwa Nyumbani Hata Kama Huna Ujuzi Wa Kompyuta.

Written by on March 22, 2018

 

Habari ya muda huu? Natumaini u-mzima kama ilivyo kwangu. Nimekuwa mwenye furaha sana leo na kwa maana hiyo ningependa kukushirikisaha habari kubwa sana ambayo naamini hakuna msanifu wa tovuti ambaye aliwahi kukueleza. Habari hii inahusu aina ya tovuti inayoweza kukuingizia pesa hata kama huna elimu yoyote juu ya kompyuta. Hakuwahi kukueleza si kwa sababu wasanifu hawa ni wabinafsi, bali ni kwa sababu kuna uwezekano mkubwa kwamba hawana ufahamu na hata ujuzi wa jambo ambalo nitakueleza muda mfupi ujao.

Wiki chache zilizopita nilipata wasaa wa kukutana na wamiliki wa tovuti katika moja ya program zangu…wengi wao walionekana kuhangaika sana (na baadhi yao, bado wanahangaika) kupata matokeo ya kile walichokusudia pasina matokeo yoyote ya kuonyesha. Kimsingi wengi wao wamefikia mkataa wa kutokuamini kama website zao zaweza kuwasaidia kutengeneza hela. Endapo nawe u-miongoni mwao, basi siku ya leo ni ya bahati kwako kwa maana naenda kubadili mtizamo wako juu ya hilo…

Ninapoongelea kutengeza pesa kutumia website yako, namaanisha kutumia website yako kama dhana ya masoko ambayo itawabadili wateja watarajiwa ambao wangependa kununua bidhaa na hata huduma kutoka kwako pasina kujali watafanya malipo kupitia website yako ama ana kwa ana. Katika mazingira yetu ya kitanzania, kimsingi ni rahisi sana kwa mtu kufanya manunuzi/malipo ya ana kwa ana hata kama website yako ndio iliyosaidia kumfanya mteja afikie maamuzi ya kununua bidhaa na hata huduma yako.[/trx_text]

Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipisicing elit, sed do eiusmod tempor incididunt ut labore et dolore magna aliqua.

[trx_text top=”20″]Katika dakika chache zijazo, utakuwa na ufahamu wa namna ambayo unaweza kutumia intaneti na hata website yako kwa manufaa (kutia pesa mfukoni mwako) na si kwa hasara (kuchukua hela kutoka mfukoni). Na haijalishi umeshajaribu mara kadhaa pasina mafanikio ama lah. Mbinu ninazoenda kukupa ni zilezile ambazo hutumiwa na watu waliokubuhu katika masoko ya mtandao ambao hutengeneza zaidi ya Tsh 600,000,000/- hadi 800,000,000/- milioni kwa wiki/mwezi katika mtandao na halikadhalika ana kwa ana.[/trx_text]
[trx_text bottom=”20″]

Vema! Hebu nikuonyeshe… Ili uweze kujenga biashara kupitia mtandao wa intaneti unahitaji kuwa na vitu hivi vifuatavyo:

 1. Website Yenye Kukuingizia Pesa
 2. Ufahamu juu ya wateja wako na tabia zao
 3. Upate watembeleaji wapya
 4. Tumia Mbinu za Kimasoko
 5. Uwe na timu ya watu wenye kukusaidia katika kazi
 6. Utengeneze mfumo utakao kufanyia kazi.

Website Yenye Kukuingizia Pesa
Ninachomaanisha ni kuwa na website ilijengwa katika mfumo ambao:

 1. Inavutia
 2. Inatafutwa kiurahisi kwenye mfumo/rafiki wa Google,
 3. Imeunganishwa kiurahisi na mitandao ya kijamii, hususani facebook,
 4. Ina foramu ya blogu,
 5. Ni rahisi kuchapisha makala muda wowote,
 6. Ina fomu ya kunasa mawasiliano ya watembeleaji waliovutiwa na bidhaa/huduma yako,
 7. Imeunganishwa na mfumo wa kuwasiliana na wateja wako kwa njia ya email.

Website Inayovutia
Kumiliki website/blogu inayovutia watembeleaji ni jambo jema, lakini kumiliki website/blogu yenye sifa tajwa hapo juu ni jambo la busara zaidi.

Rafiki wa Google
Yawezekana hapo ulipo umechanganyikiwa kwa maana huelewi ni kwa nini website/blogu yako haitokei kwenye matokeo ya juu kabisa mtu anapoitafuta kwenye Google ukilinganisha na ya washindani wako ambao kiukweli tovuti zao hazina taarifa za kutosha kama ilivyo yako. Ndiyo, hilo linawezekana kwa sababu kadhaa lakini jambo la msingi kujiuliza ni “Je, website/blogu yako iko rafiki na Google?” Injini ya kutafuta ya Google uzihadhibu na kuzipendelea baadhi ya tovuti kulingana na jinsi zilivyosanifiwa. Endapo wewe ni msanifu wa website, utakuwa unaelewa namna ya kupiga code za HTML kwa ajili ya injini ya kutafutia ya Google. Kama uelewi, bado usiwe na shaka. Kuna namna rahisi, nzuri ya kumiliki website yako ambayo imesanifiwa kwa kiwango cha hali ya juu na nitakuwa nikikuelekeza kwa kadri tunavyoendelea.

Rafiki wa Mitandao ya Kijamii, hususani Facebook
Haitaji uwe na elimu ya chuo kikuu kuweza kuelewa kuwa intaneti imekuwa kiunganishi kikubwa cha watu hususani kupitia mitandao ya kijamii kama Facebook, Twitter, WhatsApp, LinkedIn n.k na hasa ndo imekuwa kinara. Hebu tizama takwimu za hivi karibuni za watumiaji mitandao hii hawa kwa mwezi.

Kama website yako si rafiki wa mitandao ya kijamii, haina shaka kwamba utakuwa unaacha hela mezani.

Kwa lugha nyingine, website/blogu yako inabidi iwe katika mfumo ambao:

 1. Unapochapisha makala yako kwenye tovuti/blogu, moja kwa moja ionekane pia. kwenye mitandao ya kijamii.
 2. Wasomaji wako wawe na uwezo wa kuwashirikisha wengine kwa njia rahisi ya kubofya vitufe vya “Shirikisha.”
 3. Wasomaji wako wanapochangia mawazo yao, yaonekane kwenye akaunti zao za facebook.
 4. Lakini pia, iwawie rahisi marafiki kuwasiliana nawe moja kwa moja kupitia mtandao ya kijamii kama unavyoo katika blogu hii.

Rahisi Kuchapisha Makala katika Muda Wowote Unaotaka
Moja ya changamoto kubwa niliyogundua wakati naongea na wana-blogu wengi ni kuwa wanapata tatizo sana pale wanapotaka kufanya mabadiliko katika blogu zao lakini pia kuchapisha makala kwa kuwa mara nyingi wasanifu wa blogu zao muda mwingi wanakuwa hawana nafasi pale wanapohitajika.

Jambo la msingi ambalo nataka ulitambue ni kuwa UHITAJI KUWA NA MTAALAMU WA WEBSITE/BLOGU unapohitaji kufanya hayo yote (endapo tu utakuwa na teknolojia ya kisasa iliyo rahisi). Linalokupasa wewe ni kuwa na makala yako pamoja na vidole vya kuchapa makala husika. Hivyo ni jambo la busara kumtahadharisha mtaalamu wako akutengenezee website/blogu ambayo hutamuitaji endapo ukitaka kufanya maboresho yoyote. Ukiona anakuchanganya au haelewi unachomaanisha, basi achana naye…waweza kupata wataalamu walio wazuri zaidi hapa.
Fomu ya Kunasa Wateja Watarajiwa
Hii ndo dhana muhimu sana kuweza kunasa watembeleaji wa website/tovuti yako lakini jambo la kusikitisha ni kuwa wamiliki wengi wa tovuti hususani hapa nchini hawaitumii. Utafiti unaonyesha kuwa zaidi ya 80% ya watembeleaji wa website/blogu yako hawatarudi tena. Je, halitakuwa jambo jema kunasa mawasiliano ya watemebeleaji wako kwa ajili ya mawasiliano kupitia barua pepe zao? Je, halitakuwa jambo kuwaarifu watembeleaji wako juu ya offer ya bidhaa/huduma yako kupitia barua pepe zao?

Njia rahisi ya kukuwezesha kunasa mawasiliano ya wateja wako kupitia fomu, ni kuwahakikishia unawapa kitu kinachoongeza thamani kwao ili waweze kuingiza jina, namba ya simu na email. Watu hawapendi kutoa mawasiliano yao kirahisi namna hiyo. Mbinu hii inajulika kama “Masoko Kishika Uchumba” Unaweza kuwapatia RIPOTI ya BURE, MAFUNZO ya BURE kama ninayotoa mimi, na hata VIDEO ya BURE!

Wasiliana na Wateja Wako Kwa Njia ya Email
Hebu fikiria umeanza kunasa watu 10, 20, 50 na hata 100 kupitia website/blogu yako kwa siku. Fikiria katika mwaka 1/2, yawezekana kabisa ukawa na watu 100,000 katika orodha yako. Ukiwa na injini ya email kama ninayotumia mimi ya Shout out (ambayo kimsingi nakushauri uitumie), unaweza kuandaa kampeini ya email ambazo zitakuwa zikitumwa kwa watu wote 100,000 wanaopatikana katika orodha yako kwa mara moja na katika muda kwa kadri utakavyoamuru iwe. Mfumo huu utakufanyia kazi wenyewe wakati wewe ukiwa coco beach na baby/familia yako mkipata vinywaji vya baridi.

Kama website/blogu yako ina pointi zote saba nilizoeleza hapo juu, nina hakika utakuwa unapokea hela nyingi kwa siku/wiki/mwezi. Kama haina, nakushauri usiendelee kusoma. Chukua simu yako haraka sana, mpigie msanifu wa Website/blogu yako akufanyie kile nilicho kushauri.

Endapo hauridhishwi na website/blogu yako na hata msanifu wako na hivyo ungependa kupata ushauri wa BURE kutoka kwangu, nitumie ujumbe kwa ku-comment hapa chini, nami nitarudi kwako nikiwa na majibu. Lakini pia kama hauna website/blogu na ungependa kumiliki yenye sifa tajwa hapo juu, usiwaze…bofya hapa utengenezewe site yako ndani ya muda mfupi.

NB: Natoa upendeleo kwa watu wachache walioko mkoani Dar kwa ajili ya kuwapa ushauri BURE! Hii ni kwa sababu timu yetu iko busy sana na hivyo tungependa kutumia muda mwingi na wateja.

Ili kuhakikisha haukosi kukutana nami kwa ushauri wa BURE jisajiri na mtandao huu hapa kuweka nafasi yako. Kumbuka, programu hii ya kutoa ushauri wa BURE itaondelewa muda wowote kuanzia sasa.

NBB: Usisahahu ku-comment hapa chini pamoja na kuwashirikisha marafiki zako wa mtandaoni kwa kubofya moja ya vitufe hapa.

Asante kwa muda wako!

 One comment

 • Cialis generic Excellent post. I was checking constantly this blog and I am impressed! Very useful info specially the last part :) I care for such information much. I was looking for this particular info for a long time. Thank you and good luck.


Search
The Days of Making a List of Your Warm Market, Chasing Your Friends and Family, Cold-Calling Leads, and Showing the Plan... ARE DEAD!​
Use internet to build your Network Marketing business

GET STARTED HERE