Mambo Unayopaswa Kufahamu Kabla ya Kuanza/Wakati Wa Kutumia Mitandao ya Kijamii.

Written by on April 10, 2018

Napenda kuanza makala hii fupi kwa kueleza maoni toka kwa marafiki zangu wawili yaliyoibuliwa wakati wa mjadala wetu mpana juu ya matumizi halisi ya mitandao ya kijamii. Mjadala wetu huo ndo umenipa msukumo mkubwa wa kushirikisha maoni yangu hapa lengo hasa likiwa ni kutaka kupata maoni yenu pai. Hebu tuanze kwa kuyachunguza maoni haya:

“Nina marafiki wanaoishi katika nchi nyingine, na njia bora ya kuwasiliana nao ni kutumia mitandao ya kijamii. Ninafurahia kuzungumza nao hata ingawa wanaishi mbali sana.”—John, 27.

“Ninafikiri kutumia mitandao ya kijamii ni kupoteza wakati, ni njia ambayo wavivu hutumia kuwasiliana. Kuwasiliana uso kwa uso ndiyo njia pekee ya kudumisha urafiki.”—Amani, 29.

Maoni yako yanakaribiana na maoni gani yaliyoonyeshwa hapo juu? Vyovyote vile, jambo moja ni hakika: Mitandao ya kijamii inatumiwa na watu wengi sana. Fikiria hili: Ilichukua miaka 38 kwa watu milioni 50 kuanza kutumia redio, miaka 13 kwa idadi hiyohiyo ya watu kuanza kutumia televisheni, na miaka 4 kwa idadi hiyohiyo kuanza kutumia Intaneti. Lakini, hivi karibuni, katika muda wa miezi 12 tu, hadi sasa Facebook imepata watumiaji zaidi ya billion mbili!

Utafiti wa hivi karibuni unaonyesha kwamba, karibu asilimia 66 ya watu wanaotumia mitandao ya kijamii wana umri wa miaka 16 au zaidi. Katika mwaka wa 2009 idadi kubwa zaidi ya watu walioanza kutumia mitandao hiyo walikuwa na umri wa zaidi ya miaka 20!

Hata hivyo, mamilioni ya vijana hutumia mitandao hii, na kwa baadhi yao hiyo imekuwa ndiyo njia wanayopendelea zaidi kuwasiliana. “Nilifunga akaunti yangu,” anasema msichana mmoja anayeitwa Jessica, “lakini nikaifungua tena kwa sababu hakuna mtu aliyekuwa akiwasiliana nami kupitia simu. Ni kana kwamba watu wanakusahau iwapo hutumii Facebook!”

Swali la msingi kujiuliza, ni kwa nini watu wengi wanavutiwa na mitandao ya kijamii? Jibu ni rahisi: Wanadamu wana tamaa ya kiasili ya kuwasiliana na wanadamu wenzao. Na hilo ndilo kusudi kuu la mitandao ya kijamii.

Uwe Mwangalifu

Kwa njia fulani, kutumia mitandao ya kijamii kunaweza kulinganishwa na kuendesha gari. Bila shaka umejionea kwamba si watu wote walio na leseni ambao huendesha gari kwa uangalifu. Kwa kweli, watu wengi wamepatwa na aksidenti mbaya kwa sababu ya kutokuwa waangalifu au kupuuza mambo.

Ni hali moja na watu wanaotumia mitandao hii ya kijamiii. Wengine huitumia kwa busara; wengine ovyoovyo. Ikiwa umeamua uwe na akaunti katika mitandao hii, ni jambo la busara ukauitumia kwa njia nzuri. Kwa hiyo, wewe ni dereva wa aina gani? Je, umeonyesha kwamba ‘unalinda hekima inayotumika na uwezo wa kufikiri’?

Katika makala hii tutazungumzia mambo mawili kuhusu mitandao hii ambayo yanastahili kufikiriwa kwa uzito—faragha yako na wakati wako.

FARAGHA YAKO

Huenda usifikirie kwamba unahitaji kulinda faragha yako unapotumia mitandao hii. Kwa kweli, kusudi kuu la kufungua akaunti ni kuwafikia watu. Hata hivyo, usipokuwa mwangalifu utapatwa na madhara.

Kwa mfano, tuseme kwamba una pesa nyingi. Je, utawaonyesha watu wote unapotembea na marafiki wako barabarani? Kufanya hivyo kungekuwa upumbavu—ni kana kwamba ungekuwa unamwomba mtu fulani aje aziibe! Ukiwa na hekima, utaficha pesa zako mahali ambapo hazionekani.

Linganisha habari zako za kibinafsi na pesa. Ukiwa na hilo akilini, angalia orodha iliyo hapa chini na utie alama kwenye mambo ambayo hungetaka yajulikane na mtu usiyemjua.

  • mahali ninapoishi

  • anwani yangu ya barua-pepe

  • shule ninayosomea

  • wakati ambapo niko nyumbani

  • wakati ambapo hakuna mtu nyumbani

  • picha zangu

  • maoni yangu

  • mapendezi yangu

Hata ikiwa wewe ndiye mtu mwenye urafiki zaidi ulimwenguni, bila shaka utakubali kwamba kuna mambo fulani katika orodha iliyo hapo juu ambayo hayapaswi kufunuliwa kwa watu wote. Lakini vijana wengi—na hata watu wazima—wamewaambia watu wasiowafahamu kabisa habari kama hizo! Unaweza kuepuka hatari kama hiyo jinsi gani?

Unapoamua kutumia mitandao hii , unahitaji kufahamu kabisa mbinu ambazo mitandao hii hutumia kuweka siri—na uzitumie. Usidhani eti kituo mitandao hii italinda faragha yako kwa niaba yako. Ukweli ni kwamba mitandao hii imepanga mambo kwa njia ya kwamba watu wengi zaidi wanaweza kuona na kutoa maelezo kwenye ukurasa wako kuliko unavyofikiri. Hiyo ni sababu moja iliyomfanya msichana anayeitwa Allison afiche habari zake kwa njia ambayo ni marafiki wake tu wa karibu wangeweza kuona anachofanya kwenye kituo hicho.

“Baadhi ya marafiki wangu walikuwa na marafiki ambao sikuwajua,” anasema, “nami sikutaka watu hao nisiowajua wasome mambo kunihusu.”

Hata ikiwa unawasiliana na marafiki wako wa karibu tu, bado unahitaji kuwa mwangalifu. “Unaweza kunaswa na tamaa ya kupokea maelezo kutoka kwa marafiki wako,” anasema Corrine mwenye umri wa miaka 21, “na hivyo uanze kuonyesha habari nyingi zaidi za kibinafsi kuliko unavyopaswa kufanya.”

Sikuzote unapaswa kukumbuka kwamba Intaneti haina siri kabisa. Kwa nini? “Tovuti kubwa huweka nakala za habari zake,” anasema Gwenn Schurgin O’Keeffe katika kitabu chake CyberSafe, na anaongezea hivi: “Kwa kweli, mambo tunayopachika kwenye Intaneti hayapotei. Lazima tukumbuke kwamba habari zote ni za kudumu kwa kuwa kuna nakala mahali fulani; kufikiria kwa njia tofauti ni upumbavu.”

WAKATI WAKO

Si faragha yako tu bali pia wakati wako unaweza kulinganishwa na pesa nyingi. Kwa sababu hiyo, unahitaji kupanga jinsi utakavyotumia wakati wako. Na hilo ni moja kati ya mambo magumu zaidi kuhusiana na matumizi ya Intaneti, kutia ndani matumizi ya mitandao ya kijamii.

Jambo Muhimu


Kuna jambo lingine kuhusu mitandao ya kijamii ambalo unapaswa kufikiria. Ili kukusaidia uelewe jambo hilo, tia alama ya ✔ kando ya jibu unaloona ni sahihi.

Mitandao ya kijamii hasa ni . . .

(A) …….. biashara.
(B) ․․․․․ klabu cha kujumuika.
(C) ․․․․․ aina ya burudani.

Jibu sahihi ni nini? Amini usiamini ni A. Kwanza kabisa, kituo cha mawasiliano ni biashara. Kusudi lake kuu ni kupata faida, hasa kupitia matangazo ya kibiashara. Na kwa watangazaji wa kibiashara, thamani ya kituo cha mawasiliano huongezeka kadiri watu wengi zaidi wanavyojiandikisha na kadiri vitu ambavyo watu hao wanapachika vinavyosambazwa. Kwa kweli, kadiri wewe au mtu yeyote anavyotumia wakati mwingi zaidi katika mitandao, ndivyo matangazo mengi zaidi yatakavyotazamwa.

Kutambua jambo hilo kunakusaidia kutambua kwamba mitandao hii haipotezi chochote—na watangazaji wa kibiashara wanafaidika sana—unapowasambazia watu wengi sana habari au unapotumia muda mwingi sana kwenye Intaneti. Kwa vyovyote basi, ikiwa unatumia kituo cha mawasiliano, linda faragha yako na uwe mwangalifu kuhusu muda unaotumia katika kituo hicho.

Ni matumaini yangu kuwa umejifunza jambo muhimu litakaloweza kukusaidia katika matumizi ya mitandao kuanzia sasa. Katika makala zijazo nitaelelezea mbinu unazoweza kuzijtumia ili matumizi ya mitandao hii yawe yenye manufaa kwako hasa kukuingizia kipato!There are no comments yetSearch
The Days of Making a List of Your Warm Market, Chasing Your Friends and Family, Cold-Calling Leads, and Showing the Plan... ARE DEAD!​
Use internet to build your Network Marketing business

GET STARTED HERE